Karibu Kwa Website ya Nooalf

Kulingana na mwelekeo wa kisasa huenda kukawa na lugha rasmi ya kimataifa mwishoni mwa karne. Hii lugha ya kimataifa itajumulisha sehemu kubwa ya Kiingereza na msamiati mwingi kutoka lugha zingine. Karne nyingine baadaye, 2200, hakutakuwepo na lugha nyingine itakayokuwa imesalia. Ingawa utabiri huu huenda uwe wa kuhuzunisha kwa wengi, hili ni jambo zuri ikiwa watu watawasiliana kwa urahisi, basi wanaweza kuelewana kimawazo na kuwa na nafasi bora ya kuishi kwa amani. Kwa hivyo, kukiwa na ushirikiano mambo mengi yataweza kutekelezwa.

Lakini hata hivyo kuna SHIDA kubwa!

Kiingereza hakina mtindo wowote wa tahajia!
Hili jambo linafanya kujifunza kuwa kugumu. Kwa vile hakuna mtu yoyote anaweza kutaja kila neno. Kusema kweli, lugha nyingi kubwa duniani hazina mtindo wa tahajia wa kuaminika!

Kwa hivyo, suluhisho ni Nooalf

Nooalf iliundwa 1989 kuchukua mahala pa desturi ya hapo awali ya tahajia ya Kiingereza. Nooalf inajihusisha na kila sauti inayotakikana kuwakilishwa na lugha inayoongewa. Lugha hii ni lazima ionekana kuwa sawa na desturi ya kale ya tahajia inayoweza kusomeka na kila mtu kwa mara ya kwanza hata kama mtu ajawahi kuiona. Kipawa hiki kitakuwezesha kuandika maandishi yanayoeleweka kwa muda wa miezi michache badala ya kutumia miaka mingi kukariri maelfu ya miundo ya maneno isiyokuwa na maana yoyote. Kwa hivyo utaweza kutaja neno lolote bila kuchanganyikiwa ilihali msamiati wako.utaimarishwa kwa haraka. Lugha nyingi zina sauti sawa zinazopatikana kwa Kiingereza na kwa hivyo Nooalf inaweza kutumiwa kutaja maneno mengi duniani!

Nooalf ndiyo tahajia ya baadaye
Karibu kwa mapinduzi !